#SwaWed: Swahili Wednesday

[tweetmeme source=”Joliea” only_single=false]

Imerudi tena!

Na ninashangaa kama nitaweza kuiendelesha trend hii.

Lakini naona umuhimu wake. Labda sitaandika mengi kwa sababu kiswahili yangu sio nzuri lakini kujaribu kwangu kunaonyesha kuwa ninataka kuendelea kujikumbusha na kuiendeleza. Na ndio maana utaona nikifanya posti kama hii katika lugha hii.

Kile ambacho kinanisumbua sasa hivi ni kwamba mara nyingi sisi wakenya, na haswaa wakaazi wa Nairobi, hatupendi kuitumia lugha yetu ya taifa vizuri. Kile ambacho tunapenda kufanya ni kuongea katika kiingereza sana na hapa na pale tutatumia sheng na mara kidogo sana labda lugha ya mama. Lakini Kiswahili sanifu kilitupiliwa mbali.

Ata ninavyosema hivo, mimi mwenyewe najijua. Nakumbuka kule nilipokuwa nafanya kazi mbeleni wafanyikazi wenzangu walikua wana mazoea ya kutumia lugha ya mama kila wakati. Tena accent yao ilikua nzito sana hata mimi mwenyewe karibu niishike! Halafu nilipoingia kampuni hii nipo sasa, kila mtu anatumia kiingereza. Wengine ni wamarekani, na wengine ni kama wametoka bado kuko huko marekani. Kupambana nao basi ilikua ni shida mno. Mimi nilikua nimezoea sheng na kiingereza tu ile kidogo kidogo hapa na pale. Baadaye nilizoea na mambo yako shwari. Lakini kama sasa najua mwalimu yeyote ambaye ataiangalia posti hii atacheka sana akitoa makosa hapa na pale. Sijui niseme nini.

Nikitamatisha posti hili, naapa ya kwamba, nitajaribu iwezekanavyo kuiendelesha Swahili Wednesday / Swahili Jumatano.

Naapa pia nitaendelea kuijulisha na lugha hii na kujaribu kusoma vitabu vilivyoandikwa katika kiswahili ili niiendeleze na kuimarisha lugha yangu kwa kuandika na pia kwa kunena.

Naipa shukran Kamusi.org au Kamusi Project kwa kunisaidia kutafsiri maneno mengine ambayo nimeyatumia hapa.

Share

Swahili Wednesday #Swawed

[tweetmeme source=”Joliea” only_single=false]

Unalikumbuka hili kitabu?

Nilipoanza kufikiria jinsi nitakavyoandika hili posti sikujua ya kwamba itakua vigumu sana kuliandika! Ata bila kuanza, lazima ninene hapa kuwa,

Kanusho: Chochote nitakachoandika hapa sijui kama ni Kiswahili Mufti na siwezi dhamini kuwa maandishi haya yamefanywa vizuri na vile inapaswa kuandikwa. Hehe..

Leo, kama wale wote wanaonifuata kwenye Twitter wanavyojua, akina @Nbad_kitty, @Chiira, na pia @mapambo ndio walioanza na kuendelesha hili trend la #SwaWed. Ukilibonyeza hilo link utajionea mambo ambayo tunafanya. Kwa sasa bado hakuna maneno mengi ambayo yamesemwa na labda ni kwa sababu wanao twiti wamesahau. Lakini hakuna shida.

Lengo langu la kuandika hili posti ni kwa sababu lugha hili la Kiswahili kwa mara mingi husahaulika na kutupiliwa mbali. Kwa mfano, ni wangapi wetu wanaotazama habari zinazosomwa kwa Kiswahili? Natumae stesheni zote nchini huwa nazo na pia vipindi vinavyotumia lugha hii.

Kwa hivyo basi nikitamatisha posti hili, nataka kujitahidi mimi mwenyewe nijaribu vyote ninavyoweza niendelee kulitumia hili lugha ili basi ata mnamo nitakapokwenda kutembea nchi za jirani zingine kama Tanzania au Rwanda, wanaolitumia hili lugha, nitaweza kujitambua na kujijulisha vile ninavyopaswa.

Kwa kweli Kiswahili Kitukuzwe, ndio lugha ya taifa.


Share

%d bloggers like this: