#SwaWed: Swahili Wednesday

[tweetmeme source=”Joliea” only_single=false]

Imerudi tena!

Na ninashangaa kama nitaweza kuiendelesha trend hii.

Lakini naona umuhimu wake. Labda sitaandika mengi kwa sababu kiswahili yangu sio nzuri lakini kujaribu kwangu kunaonyesha kuwa ninataka kuendelea kujikumbusha na kuiendeleza. Na ndio maana utaona nikifanya posti kama hii katika lugha hii.

Kile ambacho kinanisumbua sasa hivi ni kwamba mara nyingi sisi wakenya, na haswaa wakaazi wa Nairobi, hatupendi kuitumia lugha yetu ya taifa vizuri. Kile ambacho tunapenda kufanya ni kuongea katika kiingereza sana na hapa na pale tutatumia sheng na mara kidogo sana labda lugha ya mama. Lakini Kiswahili sanifu kilitupiliwa mbali.

Ata ninavyosema hivo, mimi mwenyewe najijua. Nakumbuka kule nilipokuwa nafanya kazi mbeleni wafanyikazi wenzangu walikua wana mazoea ya kutumia lugha ya mama kila wakati. Tena accent yao ilikua nzito sana hata mimi mwenyewe karibu niishike! Halafu nilipoingia kampuni hii nipo sasa, kila mtu anatumia kiingereza. Wengine ni wamarekani, na wengine ni kama wametoka bado kuko huko marekani. Kupambana nao basi ilikua ni shida mno. Mimi nilikua nimezoea sheng na kiingereza tu ile kidogo kidogo hapa na pale. Baadaye nilizoea na mambo yako shwari. Lakini kama sasa najua mwalimu yeyote ambaye ataiangalia posti hii atacheka sana akitoa makosa hapa na pale. Sijui niseme nini.

Nikitamatisha posti hili, naapa ya kwamba, nitajaribu iwezekanavyo kuiendelesha Swahili Wednesday / Swahili Jumatano.

Naapa pia nitaendelea kuijulisha na lugha hii na kujaribu kusoma vitabu vilivyoandikwa katika kiswahili ili niiendeleze na kuimarisha lugha yangu kwa kuandika na pia kwa kunena.

Naipa shukran Kamusi.org au Kamusi Project kwa kunisaidia kutafsiri maneno mengine ambayo nimeyatumia hapa.

Share

24 Responses to “#SwaWed: Swahili Wednesday”

 1. Wamathai Says:

  Pia mimi niko kama wewe najua kuongea Kiswahili lakini mimi hutumia sheng mara mingi na nifikiri ni muhimu tujifunze kuongea Kiswahili sanihu kama vile sisi huongea Kingereza sanihu.
  Ni ruhusu nikukosoe. Hapa ungesema ‘kwa sababu kiswahili changu sio kizuri’

 2. 2chilledmalts Says:

  Hahaha, kcs (Kicheko cha sauti)! Nyinyi wawili mmenitumbuiza asubuhi, walalala.

  Kweli mwalimu wangu wa Lugha darasa la sita Bwana Ngugi angetutusi! “Maandazi!” alipenda kusema ulipokosea lugha, msamiati ama ngeli.. Mmenirudisha mbali sana!! Lakini labda ni vizuri kukumbuka – mimi nimzazi, kwahivyo hivi karibuni watoto wangu watahitaji usaidizi na kazi ya ziada, na kama sheng ndio nimejizowesha, nitawasaidiaje?

  Joliea, kuna jambo mmoja sikubaliani nawe kuhusu lugha sanifu (Wamathai sio *sanihu) ya Kiswahili. Lugha zote duniani zabadilika kila wakati. Kiswahili ni mseto wa Kiarabu, Kibantu, Kireno, Kichaina na kadhalika. Maneno mapya bado yanaongezwa; sheng ni lugha kivyake. Shida ni haina mpangilio wa msamiati. Haimaniishi ni lazima tuongee Swahili sanifu – yachosha kufikiria, sembuse kusema!

  Kiswahili changu kimeishia hapo! 🙂

  • Joliea Says:

   Hahahaaaa!!!

   Ata wewe umenifurahisha sana leo hii!

   Asante sana kwa mawaidha haya. Umesema mengi ambayo nilikuwa nayafikiria lakini kwa vile hii lugha yeto tuipendayo ni gumu mno, mara nyingine unashindwa kuitumia na unatupa mikono juu na kuwika “to hell”!! Heheee!

 3. kiokoken Says:

  hongera. Kiswahili kitukuzwe kwani ndio lugha yetu ya kwanza. watu wachache sana hutumia kiswahili na kikitumika huchanganywa na kimombo. tukikuze kiswahili kwa ajili ya kizazi kijacho..

 4. kw Says:

  Uzito wa swala hili wanifanya nishindwe jinsi ya kujibu posti yako ama kukomenti ukipenda 😀 tafsiri haya…
  mwalimu wangu wa swahili bwana gathii nikiwa shule ya msingi alinifunza maneno haya kama njia ya kuanza insha zangu..hadi wa leo sijajua maneno haya yamaanisha nini lakini niliyatumia katika kila mwanzo wa insha zote ili kurembesha ile insha ata kama insha yenyewe ilinena kuhusu paulo yule octopasi! 🙂
  hii yamaanisha kwamba niko chini sana upande wa kunena swahili lakini sadakta..nafurahishwa sana na hili gumzo kama ngoma za tum tum..naomba maulana arefreshi bongo langu anipe maneno mengi ili niweze kukomenti wiki ijao..hongera!

  • Joliea Says:

   @kw, hahahaaa!! ati uko chini sana?? hehe! hapo umeniua *KIFO* KKN!!

   Asante kwa kuwa mloyal na kukomenti kila wakati 🙂 pia naomba ufanye posti moja niweke kama “Guest Post” 🙂 shukran kwako!

 5. kw Says:

  joliea, kumbe nikiyaweka maneno ndani ya bracket wordpress inayameza ama ni kitu gani hii..
  maneno ambayo nimesema hapo juu utafsiri yalikuwa haya..kaondokea chanjagaa kajenga nyumba kakaa mwanangu mwanasiti kijino kama chikichi cha kujengea vilago na vikuta vya kupitia..
  yaonekana mimi siko chini sana wasemaje?

  • Joliea Says:

   @kw, ati nini? nakwambia mwana sijaelewa chochote lile ulilosema! hataa kidogo! KKN! (Kucheka Kwa Nguvu!)

   • 2chilledmalts Says:

    Walalala, @Kw, huyo mwalimu wenu alikuwa anawakanganya! Naambiwa vikuta vya kupita ni chochoro, ni kweli?

   • kw Says:

    @2chilledmalts ata sijui niseme nini..yaani siamini kwamba hiyo miaka yote huyu mwalimu alinifanya niandike kuhusu ati chochoro sijui za wapi zile!!nasikitika sana mie.

 6. kw Says:

  hilo ni jambo mzuri sana labda unafaa uniweke kwenye testi niandike posti kwa lugha ya swahili..ingawa sijui kama hii ni idea mzuri..ati KKN..wewe uko juu sana naona 😀

 7. Cold Turkey Says:

  Kwa mara nyingine tena, juhudi ulizonazo za kukiendeleza kiswahili zaridhisha.
  Ikiwa utaweza, soma Taifa Leo pia. Lugha nzuri na hukosi vichekesho, hasa sehemu ya “Dondoo” na “Shangazi Sizarina”
  Usije ukaacha “kupigia debe” Kiswahili. Utawavutia wengi. Hongera!!

 8. sk8rrboi Says:

  Unabahati katiba ya 2005 haikupitiashwa sababu majimbo ingetekelzwa na ungepigwa marufuku kutembea jimbo la pwani. Ninasema tu.

 9. Isaac Says:

  Asante sana wakusaji wa lugha, ni muhimu sana kukosa kwa maandishi, mafikirio na misemo ili tuwakosolewa na wenzetu. na hilo ndilo lugha hukuwa. Nakumbuka nilipomalisa shule ya upili, nilifundisha lugha ya kiswahili..sas nikiwa Amerikani, napenda kuona au kusikia wenzangu wakiongea lugha..kwangu ni furaha!!

 10. Mama Says:

  Jamani, hii posti yako imenifurahisha kweli. Nakupa pongezi dadangu. Ni kitu cha muhimu kumwona M-nairobi mwenzangu akijituma kuongea lugha sanifu. Nitajihimiza nami pia niongee lugha sanifu kwanza sasa.

  Ingawaje, ningependa kufahamu “posti” na “komenti” zapaswa kuitwa vipi? Naamini kuna njia sanifu ya kutamka maneno haya, ama vipi?

 11. Peaceluve Sheikh Says:

  Hapo Garissa tuko naye kiswahili lenye MALARIA KKKKKKK kwa mfano Madhee abaye wana maanisha kama mama

 12. olinzia Says:

  wahenga walinena kua mwacha mila ni mtumwa kwahivyo natumia fursa hii kujikomboa kwenya utumwa nilojiweka mweyewe. miaka na mikaka imepita na kila kuchao tunazidi kuiga tabia na lugha za wengine na kunasahahu kukikuza kiswahili. inafedhehesha kuona jinsi ambavyop watu wanachanganya lugha.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: