Swahili Wednesday #Swawed

[tweetmeme source=”Joliea” only_single=false]

Unalikumbuka hili kitabu?

Nilipoanza kufikiria jinsi nitakavyoandika hili posti sikujua ya kwamba itakua vigumu sana kuliandika! Ata bila kuanza, lazima ninene hapa kuwa,

Kanusho: Chochote nitakachoandika hapa sijui kama ni Kiswahili Mufti na siwezi dhamini kuwa maandishi haya yamefanywa vizuri na vile inapaswa kuandikwa. Hehe..

Leo, kama wale wote wanaonifuata kwenye Twitter wanavyojua, akina @Nbad_kitty, @Chiira, na pia @mapambo ndio walioanza na kuendelesha hili trend la #SwaWed. Ukilibonyeza hilo link utajionea mambo ambayo tunafanya. Kwa sasa bado hakuna maneno mengi ambayo yamesemwa na labda ni kwa sababu wanao twiti wamesahau. Lakini hakuna shida.

Lengo langu la kuandika hili posti ni kwa sababu lugha hili la Kiswahili kwa mara mingi husahaulika na kutupiliwa mbali. Kwa mfano, ni wangapi wetu wanaotazama habari zinazosomwa kwa Kiswahili? Natumae stesheni zote nchini huwa nazo na pia vipindi vinavyotumia lugha hii.

Kwa hivyo basi nikitamatisha posti hili, nataka kujitahidi mimi mwenyewe nijaribu vyote ninavyoweza niendelee kulitumia hili lugha ili basi ata mnamo nitakapokwenda kutembea nchi za jirani zingine kama Tanzania au Rwanda, wanaolitumia hili lugha, nitaweza kujitambua na kujijulisha vile ninavyopaswa.

Kwa kweli Kiswahili Kitukuzwe, ndio lugha ya taifa.


Share

Advertisements

18 Responses to “Swahili Wednesday #Swawed”

 1. Denis Nzioka Says:

  Lahaula! Lugha ya Swahili i ngumu mno! Tufanyeje tubunishe na kuirembesha lugha hii yetu ya Taifa? Ni wajibu wa kila mtu kuibobea na kufurahia lughya yake ya mama.

  • Joliea Says:

   @Denis, Naona kana kwamba hii ni mara yako ya kwanza ku-commenti katika site hili langu! Ahsante sana. Sasa, hapo umeongea kama wanaume tano! Lakini lazima sisi wenyewe tujitolee kuliendeleza na kuitumia katika gumzo zetu za kila siku, au sivyo?

 2. cdohnio Says:

  I won’t even lie, I have read shit here! Swa is not my language, let me try use google translate:-D

  • Joliea Says:

   @cdohnio, mwanagu, si wewe bado mchanga, umetoka shuleni juzi tu! Mbona hivi? Jameni! Watoto wa siku hizi!!!

   Haha! 😀

 3. coldturkey Says:

  Duh! Nimependezwa sana sana na hatua hii ya kuandika kwa kiswahili. Ujumbe wako unaeleweka. Hongera!! Asante.

  • Joliea Says:

   @coldturkey, Karibu sana. Hii ni lengo langu kujaribu kulielewa vyema na kulitumia lugha hii ya fasaha

 4. welly Says:

  Ahsante sana Jolie kwa kujitahidi kutumia lugha ya Kiswahili.Kama umekuwa makini,basi utaona madhara ya sheng na lugha zingine yalivyosheheni na kuharibu ufasaha wa lugha hii kwa vijana.Ni wajibu wetu kuitunza na kuiendeleza lugha hii yetu ya taifa kwa ajili ya vizazi vijavyo.Ahsante.

  • Joliea Says:

   @welly, asante sana kwa kucomment 🙂

 5. Birdland Says:

  Ngeli ya kitabu ni Ki-Vi. Kwa hivyo sentensi yako ya kwanza iliyo chini ya picha ya kamusi ingefaa kuwa “Unakikimbuka hiki kitabu?”
  Vyema lakini.

  • Joliea Says:

   @Birdland, haha! hapo umeshasema ukweli. Na ndio maana tunafaa tuendelee kujikumbusha mambo kama haya.

 6. sk8rrboi Says:

  Tell you what, ur swa sucks! But 10 for the effort.

  • Joliea Says:

   @sk8rrboi, Mschew! Si niliweka disclaimer hapo? Haujaiona? Hehe…asante.

 7. Swahili Language and Culture « e377 Says:

  […] Swahili Wednesday #Swawed Me I ThinkGlobal Voices in English Africa: Free Kiswahili synthetic voice … […]

 8. Marvin Tumbo Says:

  I swear I read Swa slowly like a Class 2 kid. I am sure writing it will take forever too coz I think in English and would to go through the hassle of translating before writing. Ands that’s another story.

  Nice piece of writing though. The bit I got anyway :).

 9. uaz truly Says:

  Hehehe..kwa kweli umebobea bobu bobu katika uandishi wa lugha ya taifa.maybe u kan gv mi swa lessons:-)

  • Joliea Says:

   @uaz truly, wish it wa that easy

 10. coloseum Says:

  uz MAD!!! funny stuff..kiswahili ilikuwa ya exam tu..

  • Joliea Says:

   @coloseum, wacha kujidanganya! Utashangaa mnamo siku itakuja na utalazimishwa kuitumia lugha hii! Ata mimi bado najaribu kuitengeneza kidogo kidogo hehe.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: